Thursday, August 12, 2010

Mwandishi ajitoa kuwania udiwani


Na mwanablog wetu Dar

ALIYEKUWA mgombea wa udiwani katika Kata ya Magomeni, Dar es salaam kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),  Andrew Chale (24),  ;pichani' amejitoa katika kinyang'anyiro hicho ili kunusuru kukigawa chama.
 

Chale ambaye ni Mwandishi wa habari wa Tanzania Daima alisema jana kuwa amefikia uamuzi huo na kukubaliana na viongozi wa CHADEMA Kata ya Magomeni, ili kupisha malumbano na badala yake kuimarisha mshikamano na kuhakikisha ushindi unapatikana katika kata hiyo.

 

"Naamua kujitoa katika kinyang'anyiro, na sasa nitakuwa kampeni Meneja wa kata yangu na nihakikisha nafanya kampeni ili mteule wa chama chetu ashinde nafasi hii" alisema Chale.

 

Kwa upande wake, Katibu wa CHADEMA Jimbo la Kinondoni, Fredy Kimati, alisema chama chao wamedhamiria kushinda uchaguzi na tumekubaliana na wagombea wote akiwemo Chale, ambaye alijitoa kugombea, ili kumpisha mgombea mwenzake.

 

Hata hivyo alisema wamefanya uteuzi katika kata za Magomeni ambaye Mgombea wake Said Omary, Hassan Hussen(Mzimuni), Abdul Kazuba(Ndugumbi), Alfan Kiumbe(Tandale), Juma Ulole(Kijitonyama), Khadija Baga(Mwananyamala), Richard Rifan(Kigogo) na Njiti Mosha(Hananasifu).

 

Aidha Kimati alisema CHADEMA jimbo la kinondoni wamedhamiria kushinda uchaguzi na watahakikisha wanafanya uteuzi katika kata zilizobaki na kuwataka wananachi kuwaunga mkono katika kuimarisha demokrasia ya kweli nchin.


1 comment:

Anonymous said...

kaka unatisha naona mwaka huu kazi ipo!!!!!!!!!!!!
mwakani kama kawa nami nitakuwa kampeni meneja wako

poa ni mimi jamaa yako othman

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa