Wednesday, August 18, 2010

CCM-MAFIA WABAKI NJIA PANDA!!


 

     "Wahoji kukatwa kwa Omary Kimbau, wataka ufafanuzi"


      Na mwanablog wetu


KATIKA hali isiyo ya kawaida wananchi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mafia wapo njia panda ndani ya chama hicho kufuatia kutopatiwa ufumbuzi wa juu ya mgombea wao aliyeshinda kura za maoni na baadala yake Halimashahuri kuu ikampitisha mgombea mwingine.


 Pichani;Omary Ayubu Kimbau (katikati)akisalimiana na   Ridhiwan Kikwete(kulia) kushoto ni Idd Azan mgombea ubunge jimbo la Kinondoni.


Wakiongea kwa nyakati tofauti mapema jana  kundi la wanachama wa CCM wilani Mafia, walipinga hatua ya kamati hiyo kuliondoa jina la Omary Kimbau aliyeshinda kwa kupata kura 1803 huku mpinzani wake ambaye alikua mbunge wa  jimbo hilo Abdul Shaha akipata kura 1798.


Katika kile kilichoonekana kamati hiyo kucheza mchezo mchafu kwa Kimbau, wanachama hao walidai kuwa walitakiwa kupewa maelezo ya kina kwani wao walimchagua kwa moyo mmoja iliawatumikie jimboni hapo.


"Kwa kitendo hichi hamna sababu za kuwa na kura za maoni kwani mpaka sasa wameshindwa kuonyesha haki na thamani yetu wanaccm ndani ya chama kumpendekeza mtu tunayemtaka" alisema kiongozi mmoja wa chama hicho kutoka Kata ya Baleni amba akutaka jina lake liandikwe mtandaoni


Mbali hilo, baadhi ya wanachama wa kutoka kata ya  Kilindoni, Ndagoni,kigani,bweni na mburani wameamua kuweka mgomo baridi ilikushinikiza uongozi huo kutolea majibu ya kina na ya msingi juu ya kukata kwa jina hilo la Kimbau na kisha kulipachika jina Shaa la kuchukua maamuzi mazito ndani ya chama.


"Tunashazwa na ili lililofanywa na Kamati kuu kamwe halivumiliki kwa namna yoyote ile, tukimuuliza Kimbau anajibu tumuachie Mungu hii inatufanya tubaki njia panda tunaomba haki itendeke' alisema kada huyo aliye jitambulisha kama katibu wa Kata ya Ndagoni hakutaka jina lake lichapishwe mtandaoni


Hata hivyo alipotafutwa  Kimbau kuongelea mstakabari wa mambo kufuatia hatua hiyo ya kamati kuliondoa jina lake, hakua tayari kuongelea swala hilo na kumtaka mwandishi wa habari hizi akamuulize Katibu mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba ama Chiligati.


"Mimi sipo tayari kuongea na waandishi, hivyo juu ya swala langu kwa kina kamuulize Makamba ama Chiligati'  Kimbau aliongea kwa upole na kukata simu.


Awali Kimbau alisisitiza kuwa hayupo tayari kuliongelea swala hilo yeye amemuachia Mungu lakini haki yake hipo na anajua kwa uwezo aliyonao atafanikisha kusonga mbele na kukiimalisha chama.


Hali ya mambo ndani ya CCM tokea hatua za upigaji wa kura za maoni kumekua kukifukuta huku kila aliyeshindwa akimtuhumu mwenzake kua alicheza rafu, lakini kitendawili likamalizwa Dodoma na kamati hiyo ya NEC-CCM kwa kupitia rufani na malalamiko ya wagombea wote na kuchuja baadhi ya majina.


Kati ya majina yaliyochujwa licha ya kushinda ni pamoja na Hussein Bashe jimbo la Nzega ambapo ilidaiwa kuwa si raia kwa jimbo la Iringa Mjini, Fredrick Mwakalebela alienguliwa kwa sababu ya kua na kesi ya rushwa ambapo wanachama walitoa lawama mbalimbali juu ya hilo kwa kuonewa.



No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa