Thursday, July 29, 2010

Mgombea awapasha wapiga kura kuwa;wasipomchagua watakua kama ngedele polini

Na Mwanablog wetu Dar

HALI ya vituko na vijembe kwa baadhi ya waomba ridhaa ya kupitishwa kuchaguliwa kuwakilisha jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeendelea tena baada ya mgombea kutinga ukumbini na mikwara akiwa ametokea Mahakamani alipokua akifuatialia kesi yake ya msingi aliyoifungulia Serikali.

Tukio ilo lilitokea jana wakati wagombea hao wakijinadi katika Kata ya Mzimuni ndani ya Ukumbi wa lango la Jiji,  hata hivyo mratibu wa msafara hwa wabunge hao, Ally Kitwana aliwatambulisha wagombea wote wa wabunge  waliofika huku wawiliwakiwa hawajafika.... lakini ghafla baada ya wagombea hao kuendelea kujinadi, mgombea Nkuruma Omari Munjoli 'Nguvu ya wanyonge' alifika ukumbini hapo akiwa na suti huku akitlilika jasho na kusema kuwa ametoka mahakamani kufuatilia kesi yao ya msingi waliyoifungulia Serikali.

"WanaCCM wenzangu, hivi munavyoniona nimetoka mahakamani kufuatilia kesi ya msingi kwa ajili ya kuwatetea wananchi wa magomeni Kota, kwa nguvu niliyonayo nikiwa kama mwenyekiti wa kamati nimefanikiwa kusimamisha shughuli zote za ubomoaji wa nyumba za magomeni kota hivyo naombeni munichague iliniweze kuwatumikia zaidi na zaidi kuwatetea matatizo yenu mbalimbali huu ni mwanzo tu msipo nichagua baadae muta kiona kila mkazi wa jimbo la Kinondoni kuna hatihati ya kuamishwa na kupelekwa mapolini kama ngedele" alijinadi nkuruma.

Mgombea huyo aliwataka wananchi wa Magomeni na wa jimbo hilo kuwa makini kwani CCM ya sasa si ya henzi ya Mwalimu ambapo walithamini hutu kama ilivyo kuwa kwa azimio la Arusha na baadala yake sasa wanathamini vitu na kuingiza biashara katika Siasa.

"Haki itapatikana kwa njia mbili, mtutu ama kwa sanduku la kura, kazi kwenu kama mtanichagua mlalahoi mwenzenu ama mafisadi na wafanyabiasha matapeli" alimalizia Nkruma.

Aidha kwa upande mwingine Mgombea Mpoki Mwamburukutu aliwaomba wanaCCM kuchagua pumba na mchele kipindi hichi cha kumchagua mgombea ambaye atauuzika pamoja na kupambana na wapinzani jimboni."Jamani nimesoma mpaka kupata digrii nne kwa fedha zenu watanzania, hivyo naombeni kura yenu nirudishe fadhira, musirubuniwe jamani mchague wenyewe pumba na mchele' alijinadi Mpoki.

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa