kwa msaada wa global publisher
Miss Temeke 2006/07, Jokate Mwegelo amevunja ukimya na kuongelea uhusiano wake na Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ baada ya minong’ono kuenea kitaani kuwa wawili hao ‘wanatoka’ pamoja.
Mleta habari wetu (jina kapuni) alisema kwamba, Jokate na Chid wamekuwa wakionekana katika viwanja mbalimbali vya Jiji la Dar wakifuatana kama njiwa jike na dume.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ukaribu wao umewafanya watu wanaowafahamu kuwa na shaka kwamba inawezekana kuna kitu kinaendelea kati yao.
Baada ya habari hizi kutua juu ya dawati la Ijumaa, ripota wetu alimwendea hewani Jokate na kumpa ‘ishu’ nzima ambapo aliweka wazi kila kitu na kuhoji mtu aliyezalisha umbeya huo.
“Jamani nani aliyewaeleza hizo habari? Kwani Chid mlipomuuliza amesemaje?” Alihoji Jokate na kuangua kicheko.
Staa huyo aliongeza kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na ndiyo kwanza alizisikia kutoka kwa Mwandishi Wetu, akaongeza kuwa waliozileta ni washambenga.
Alipobanwa kwamba, kuna picha walizopiga na Chid, alisema kama zipo zitakuwa za kawaida tu za salamu na kusisitiza kuwa, yeye na msanii huyo wa kiume ni marafiki wa kawaida kama ilivyo kwa wengine.
“Wewe ni mwandishi wa gazeti gani?” Alipotajiwa, alisema kuwa yeye hajui chochote, kisha akakata simu.
Miss Temeke 2006/07, Jokate Mwegelo amevunja ukimya na kuongelea uhusiano wake na Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ baada ya minong’ono kuenea kitaani kuwa wawili hao ‘wanatoka’ pamoja.
Mleta habari wetu (jina kapuni) alisema kwamba, Jokate na Chid wamekuwa wakionekana katika viwanja mbalimbali vya Jiji la Dar wakifuatana kama njiwa jike na dume.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ukaribu wao umewafanya watu wanaowafahamu kuwa na shaka kwamba inawezekana kuna kitu kinaendelea kati yao.
...Jokate
“Kwa jinsi walivyo karibu wale watakuwa wapenzi tu, maana kila kiwanja huwa pamoja, hata hivyo ni kuwaombea heri kwa Mungu ili kama vipi waje waoane wasiwe kama wenzao wanaokuwa katika uhusiano bila malengo mazuri,” alisema mtoa habari wetu.Baada ya habari hizi kutua juu ya dawati la Ijumaa, ripota wetu alimwendea hewani Jokate na kumpa ‘ishu’ nzima ambapo aliweka wazi kila kitu na kuhoji mtu aliyezalisha umbeya huo.
“Jamani nani aliyewaeleza hizo habari? Kwani Chid mlipomuuliza amesemaje?” Alihoji Jokate na kuangua kicheko.
Staa huyo aliongeza kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na ndiyo kwanza alizisikia kutoka kwa Mwandishi Wetu, akaongeza kuwa waliozileta ni washambenga.
Alipobanwa kwamba, kuna picha walizopiga na Chid, alisema kama zipo zitakuwa za kawaida tu za salamu na kusisitiza kuwa, yeye na msanii huyo wa kiume ni marafiki wa kawaida kama ilivyo kwa wengine.
...Chid
Baada ya Jokate kutoa maelezo yake, Paparazi Wetu alimwinulia mkonga wa simu Chid Benz na kuhoji juu ya uhusiano wake na Jokate ambapo hakuwa na mengi zaidi ya kuhoji:“Wewe ni mwandishi wa gazeti gani?” Alipotajiwa, alisema kuwa yeye hajui chochote, kisha akakata simu.
Tags: ijumaa
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa