Na mwanablog wetu Dar
KAMPUNI ya Majembe Auction Mart ya mjini Dar es salaam inashikiria mali kadhaa zikiwemo magari ya kikundi cha sanaa "Tanzania One Theatre " TOT" kinachomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kushindwa kulipa deni la zaidi ya milioni 30 ilizokopa katika Benki ya Mwananchi wa Dar es Salaam .
Majembe walifika Mwananyamala kwa Mwijuma yanapopaki magari ya kundi hilo na kufanikiwa kuondoka na magari mawili likiwemo gari linalotumiwa kwa shughuli za kampeni za chama hicho, lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 596 AJB pamoja na Fuso ambalo namba zake hazikuweza kupatikana mara moja.
Kwa mujibu wa vyanzo vya mashuhuda walidai kuwa waliwashuhudia maofisa wa Majembe wakiingia ndani ya ofisi ya CCM na kuongea mambo kadhaa na walipotoka waliweza kuondoka na magari hayo yote mawili.
"Tulishikwa na hamaki baada ya kuona magari haya yakichukuliwa na Majembe, mara ghafla aliweza kutoka John Komba huku akiongea na Majembe mambo fulani fulani" kilisikika chanzo cha Habari.
Habari zaidi pia ziliweza kushuhudia kati ya magari hayo mawili, Lori hilo likiwa limeegeshwa nje ya yadi hiyo katika ofisi za Majembe makao makuu huku gari aina ya Fuso likiwa limeegeshwa ndani ya Yadi.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa Majembe Seth Motto kuhusiana na swala hilo , alikili juu ya kampuni yake kuyashikilia magari hayo, na kudai kuwa wataendelea kushikilia magari hayo mpaka wadaiwa watakapokamilisha taratibu za kuyagomboa.
Vyanzo vya kuhaminika kutoka ndani ya ofisi ya mkurugenzi huyo zilidai kuwa wanayashikilia magari hayo mpaka mwisho wake, watakapo kamilisha taratibu za malipo"
Hata alipotafutwa mkurugenzi na mmiliki wa kundi hilo la TOT, Kpt John Komba kuhusiana na tuikio hilo alikiri kutokea na kusema atalifanyia kazi likiwemo swala la kuyakomboa mapema.
"Ni kweli magari hayo yamekamatwa na Majembe, hikufuatia kudaiwa kiasi cha shilingi milioni 30, zilizokopwa benki ya Wananchi wa Dar es Salaam ." Alisema Komba
Katika maelezo yake, Komba alidai kuwa wafanyakazi wa kundi lake hilo walikopa fedha katika benki hiyo huku TOT ikiwa ndiyo mdhamana mkuu.
"Wafanyakazi wangu walikopa fedha hizo, lakini mpaka sasa wengine wameshakufa,wameama kundi na wengine wapo njee ya nchi na kusababisha deni hilo , hivyo kila mtu anadaiwa hapa sio TOT hata Serikali inadaiwa mabilioni" alidai Komba.
Aidha, Komba alikanusha juu ya mali hizo zinazoshikiliwa na Majembe na kusem akuwa si mali ya CCM wala yake bali ni ya TOT.
"Zimekamatwa mali za TOT sio za CCM, hii sio mali yao ni mali ya kampuni na inaendeshwa na kampuni ya TOT, hivyo mali zilizokamatwa ieleweke kuwa si za Chama" alisisitiza Komba.
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa