Mkuu wa Wilaya Mh. Manzie Mangochie akiwa na kofia ya njano
Na mwanablog wetu Mafia
UPEPO mkali umekikumba kisiwa cha Mafia na kuhezua nyumba 53 na kusababisha maafa kwa wakazi wa Kaya 135 kukosa Makazi na wengine saba kujeruhiwa vibaya.
Akizungumza na bog hii leo asubuhi Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Manzie Mangochie alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki April 28 majira ya saa nne asubuhi na kupelekea maafa kwa Kaya hizo 135.
Mangochie alisema kuwa, upepo huo ulitokea upande wa Kusini kuelekea Magharibi ndio uliothababisha maafa hayo kwa kuhezua mabati ya nyumba hizo takribani 53 pamoja na kuharibu mazao kadhaa ikiwemo minazi.
Baada ya kutokea tukio
"Baada ya kutokea kwa tukio ilo, sote tulifika eneo la tukio na kutoa msaada, kwa kweli lilikuwa la aina yake, napenda kuwatoa hofu wakazi waliokumbwa kuwa, kile sio Kimbunga kama walivyo dhani, bali ni upepo mkali "Cyclone" hivyo wasio hofu Mamlaka ya hali ya hewa wataendelea kurtoa taarifa zaidi juu ya hilo' alisema Mangochie.
Mangochie aliyataja maaeneo yaliyokumbwa na Upepo huo kuwa; Kilungeni A, Vunjanazi na
Pia majeruhi waliokumbwa ni pamoja na wanafunzi wanne wa shule ya msingi Kilimahewa Wasichana, walikimbizwa Hospitali na hali zao zinaendelea vizuri na wengine wawili walipatwa mishtuko na mmoja alivunjika mguu baada ya kuangukiwa na tofari.
Kisiwa hicho cha Mafia, hali ya hewa ni mvua kali karibu wiki nzima sasa, licha ya kimbunga hicho, pia mvua hiyo inayoendelea kunyesha imesababisha baadhii ya sehemu za mji huo wa Kilindoni maeneo ya Majengo kujaa mafuriko.
Mangochie alisema kujaa kwa maji hayo yaliyosababisha mafuriko, yalitokana na kuziba kwa mifereji mingi katika maeneo kadhaa ya mji huo.
Kitokea kwa tukio
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa