Thursday, May 13, 2010

KILI TAIFA CUP YAGEUKA UWANJA WA VITA IRINGA

PICHANI

Askari  polisi  wa kituo cha Iringa  wakituliza fujo kati ya wachezaji wa  timu ya Kinondoni na Mapinduzi stars kutoka Mbeya baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa mwisho wa Kili taifa Cup uliokuwa ukichezwa katika uwanja wa Samora jana na timu hizo kutoka  bila  kufungana  huku Iringa  ikiwa bingwa wa kituo hicho kwa kuifunga Rukwa kwa  goli 6-0.




Mashindoni ya Kili Taifa Cup kituo cha Iringa  yamelazika kwa  mapigano makali kati ya   wachezaji wa timu ya Mapinduzi Stars  kutoka mkoa wa Mbeya na Kinondoni baada ya timu hizo kutoka sare na kutuhumiana kupokea rushwa kutoka kwa wenyeji Iringa.
 
Mapigano hayo ambayo  yalipelekea polisi kuingilia kati huku baadhi ya askari polisi  wakitumia mikanda  ya suruali zao  zao kutumia kama silaha za kuwasambaza  mashabiki na wachezaji hao ambao walikuwa katika vita kali ya kurushiana mawe  huku wanahabari wakipokea kipigo  kutoka kwa wachezaji wa Kinondoni ambao walionekana kugeuka mbogo  baada ya kupoteza ubingwa katika kituo hicho .
 
Mwandishi wa habari hizi ambaye alikuwa ni mmoja kati wa  wanahabari  waliopokea  kichapo kutoka kwa wachezaji wa Kinondoni ambao  walikuwa wakiwaadhibu  wahasimu wao Mbeya  kwa madai ya  kuuza  kupokea rushwa kutoka kwa Iringa ili  kukaza katika mchezo kati yake ya Kinondoni.
 
Katika  vurugu hizo zilizodumu kwa zaidi ya dakika 20 baada ya mchezo  huo kumalizika  polisi zaidi ya  10 ndio ambao  walikuwepo uwanjani hapo huku  wakiwa mikono mitupu bila kirungu wala silaha yoyote ya kutuliza ghasia ,waliweza  kupata wakati mugumu  kutuliza vurugu hizo ambapo baadhi yao walipata kipigo kutoka kwa mashabi hao ambao walikuwa wakirusha mawe.
 
Baadhi ya mashabiki wa soka  wa timu ya mkoa wa Iringa  wakiongozwa na Shukuru Lwambati  walilazimika kujitumbukiza katika vurugu hizo ili kuwasaidia kuwaokoa wachezaji wa Mbeya ambao walikuwa wamezidiwa nguvu na vijana  hao wa Kinondoni katika vurugu hizo.
 
 
Wakizungumza baada ya mchezo huo mashabiki wa soka wa timu ya mkoa wa Iringa  mbali ya kuipongeza timu yao kupita kwa kishindo cha magoli 6-0 dhidi ya Pinda Boys (Rukwa ) katika mchezo wake wa mwisho na kuifanya timu hiyo ya mkoa wa Iringa kuwa  timu pekee katika kituo hicho kwa kuwa na pointi nyingi na magoli 9 na pointi 10 ikifuatiwa na Kinondoni yenye magoli  5.
 
Mashabiki hao walisema kuwa  sababu ya kinondoni kufanya fujo ni kutokana na kujiwekea malengo makubwa ya kushindwa katika kituo hicho jambo ambalo limeonekana kwenda ndivyo sivyo baada ya wenyeji Iringa kushinda na kuwa bila viongozi wa Kinondoni  kuhamasisha wachezaji wao kufanya fujo katika uwanja huo wa Samora damu zisingemwagika .
 
Hata hivyo  katibu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa (IRFA) Eliud Mvella  alipofuatwa na mwandishi wa habari hizi ili kuzungumzia fujo hizo aligoma kuzungumza na kuishia kutamka maneno mawili pekee ambayo ni No Coment.
 
Hizi ni fujo za pili kufanywa na Kinondoni toka kuanze kwa mashinadno hayo ambapo fujo zinazolingana na hizo walizifanya wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo baada ya kutoka sare ya goli 1-1 na Iringa na hivyo kufanya fujo mbele ya mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz pamoja na katibu mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela







No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa