Tuesday, May 18, 2010

 DEMOCRATIC PARTY  "DP"  SAA YA UKOMBOZI SASA

 

YATANGAZA TARATIBU ZA KUCHUKUA FOMU

 

 Mwenyekiti wa DP, M. C. Mtikila

 

Na Mwanablog wetu

 

 

CHAMA Cha Democratic Party (DP) kimetoa utaratibu wa  kupata wagombea  wa Urais,Ubunge,Udiwani na  Viti maalum kwa ajili ya Uchaguzi wa Mkuu wa 2010 huku fomui ya mgombea Urais ikipatikana kwa shilingi 50,000.

 

Katika taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na mkurugenzi wa Uchaguzi,M.Mchunguzi ilisema kuwa fomu hizo za mgombea Urais anatakiwa kulipia kiasi cha shilingi 50,000 na anatakiwa kuwa na wadhamini 200 kutoka katika mikoa 16, Tanzania bara na Visiwani.

 

Ilieleza kuwa, fomu hizo zitatolewa kuanzia Juni 15 makao makuu ya chama hicho na kutakiwa kuirudisha Julai 15, ambapo kwa hatua hiyo ni pamoja na Zanzibar .

 

Muchunguzi alisema kwa upande wa Wagombea Ubunge na Uwakilishi watapata fomu hizo kupitia katika ofisi za majimbo huku kila mgombea anatakiwa kuwa na wadhamini 60, na fomu itakuwa shilingi 10,000 mbali na hilo, kwa wagombea wa Udiwani watachuklua katika ofisi za Kata huku wakitakiwa kuwa na orodha ya majina 40 na gharama ya fomu ikitolewa kwa shilingi 5,000.

 

Makundi mengine yatakayobahatika kupata fomu hizo bila malipo ni pamoja na wagombea wa viti maalum vya Ubunge/Uwakilishi na Udiwani ambao wao watatakiwa kuwa naa wadhamini husika.

 

Aidha, katika taarifa hiyo ilieleza kuwa, makundi ya Wanawake,Vijana na Walemavu hawatagharamia fomu.

 

 

 


No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa