WATU watatu wamerafiki dunia papo hapo na wengine zaidi ya saba kujeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la Lobian Express kuvamia Lori la Mafuta mkoani Singida.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa tisa alasiri baada ya tairi la mbele la basi hilo kupasuka, wakati dereva wake akijaribu kulipita Lori lenye namba za usajili T268 TRC, likiwa na Tela lake.
Chanzo cha ajali hiyo ni mwenda kasi ambapo dereva wake alishindwa kulimiliki basi kutokana na kupasuka tairi la mbele.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, basi hilo lenye namba za usajili T637 AWD, lilikuwa likitokea Singida na kuekea Manyoni ambapo lilipofika maeneo ya Kamalula jimbo la Manyoni Mashariki, lilipasuka tairi lake kitendo kilichofanya dereva wake kushindwa kulimiliki na hatimaye kugonga Lori la mafuta.
"Lilikuwa likitokea Singida na kuekea Manyoni ambapo lilipofika maeneo ya Kamalula, jimbo la Manyoni Mashariki, lilipasuka tairi la mbele na kuanza kuyumba na hatimaye kuligonga Lori" vilisema Vyanzo hivyo.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, abiria wa kwenye basi hilo alifariki dunia papo hapo na wengine kujeruhumiwa vibaya.
Kiliongeza kwamba, pia watu wawili wa kwenye Lori walifariki papo hapo.
Chanzo hicho kiliongeza, maiti ya watu hao imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni ambapo bado hawajatambuliwa.
Aidha, abiria waliojeruhumiwa wamekimbizwa kwenye hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu zaidi.
Chanzo cha habari kilisema kwamba, baada ya tukio hilo madereva wote walikimbia.
Hata hivyo liijaribu kuwasiliana na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Singida Celina Kaluba, kuhusiana na tukio hilo ambapo simu yake haikuweza kupatikana.
No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa