UPIGAJI 'KIPUSA' MARUFUKU SHULENI SOMALIA
![]() | ||||
Waalimu katika mji mmoja nchini Somalia wamesema wanaharakati wa Kiislamu wameamrisha shule kuacha mara moja kutumia kengele kutenganisha kipindi kimoja na kingine wakati wa masomo shuleni. Wapiganaji hao wamesema milio ya kengele hizo ni sawa na ile inayosikika makanisani. Mwalimu mmoja ameambia BBC kundi la Al Shabaab limesema waalimu wa shule zitakazokaidi amri hiyo watapelekwa mbele ya mahakama za Kiislamu ama Sharia. Mwalimu mkuu kutoka shule moja amesema kundi la Al Shabaab pia limeamrisha historia ya vita vya Jihad kuwekwa kwenye mitaala. Tayari kundi hilo limepiga marufuku muziki kupigwa katika maeneo inayodhibitili na pia redioni. | ||||

No comments:
Post a Comment
here u,re comments/acha ujumbe wako hapa