Sunday, April 11, 2010

Raia wa Sudan wapiga kura katika uchaguzi mkuu
 
 
Wapiga kura nchini Sudan wanaelekea kwenye vituo vya kupigia kura katika uchaguzi wa kwanza kufanyika katika kipindi cha miaka ishirini na minne.

Wanasiasa kadhaa na vyama vinavyompinga Rais Omar al-Bashir wanasusia uchaguzi huo kutokana na hofu ya kutokea kwa wizi wa kura.

Watu zaidi ya millioni kumi na sita wamejiandikisha kushiriki uchaguzi huo wa urais, mikoa na majimbo, ambao unatarajiwa kuendelea kwa muda wa siku tatu.

Uchaguzi huo unafanyika kama sehemu ya mkataba wa amani uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo miwili kati ya kaskazini na kusini.

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter, ambaye yuko nchini Sudan, amesema anatarajia uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Bw Carter alisema ana matumaini ya kuona wananchi wakipiga kura bila woga wala vitisho, na uchaguzi kufikia viwango vya kimataifa.


No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa