Wednesday, April 28, 2010


OBAMA AMTUMIA JK SALAMA ZA MUUNGANO


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amepokea salamu za Pongezi kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani na Aga Khan Kiongozi wa wa Ismailia duniani kwa kusherehekea Sikukuu ya Muungano iliyoadhimishwa jana nchini kote.

"Mpendwa Rais, kwa niaba ya watu wa Marekani, nakutumia salamu zangu za dhati kukupongeza wewe na watu wa Tanzania, wakati mnaposherehekea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26, April" imesema sehemu hiyo ya taarifa iliyopitia Ubalozi wa Marekani hapa nchini.

"Ni matumaini yangu kwamba miaka ijayo italetea Watu wa Tanzania Amani na mafanikio ya kudumu".  Rais Obama amemueleza Rais Kikwete katika salamu hizo na kuelezea nia yake na matarajio ya baadaye kuwa nchi hizi zitaimarisha mahusiano baina yao kwa kusema  "Natarajia tutaimarisha na kuwa na mahusiano thabiti  baina ya nchi zetu," salamu za Rais Obama  zimeeleza.

Nae Kiongozi wa wa Ismailia duniani amemueleza Rais Kikwete furaha yake na kutoa salamu za Kheri kwa Rais Kikwete na Watanzania wote.

"Wa-Ismailia Imamat na Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, kwa pamoja tunaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania na  Jumuiya za Kiraia katika kuchangia  katika ukuaji wa nchi na nafasi kwa watu wote wa Taifa".  Ameeleza na kumshukuru Rais Kikwete kwa ushirikiano wake.

"Tunathamini ushirikiano wako na wa Serikali yako katika kuunga mkono na kutia moyo shughuli za Jumuiya ya Aga Khan" Salamu  za Aga Khan zimeelezea.

 

Imetolewa na Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,

IKULU-DSM




No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa