Monday, April 5, 2010

MSANII 'LEO' KUINGIZA 'UMENITEKA' VIDEONI

 

 

MSANII nyota wa muziki wa Kizazi kipya nchini, Said  Ally  'LEO'  anayetamba na kibao cha 'Waliotabiri' yupo katika harakati za mwisho za upigaji wa picha za video wa wimbo wake mpya utakaojulikana kwa jina la "Umeniteka".

 

Akizungumza  jijini Dar es Salaam,  LEO alisema kuwa, taratibu zote za kutoa wimbo huo katika video zimekamilika. "Jumamosi hii tunaingia location, na kupiga baadhi ya vipande vya  wimbo huu ambapo tutapiga kila maandhari ilikuendana na sura ya wimbo na ubora wa hali ya juu" alisema.

 

Akifafanua zaidi juu ya ujio wa video ya wimbo huo wa 'Umeniteka' uliokatika maadhi ya Zuku na Lege huku ndani yake akimshilikisha Idd au Sanko B, ambapo katika harakati za kuinua sanaa hiyo Nchini,LEO aliwaomba wadau waisubiri kwa hamu video hiyo ambayo itakuwa ni ya kitofauti na video nyingine hapa nchini.

 

"Wadau wakae mkao wa kula, video hiyo inatalajia kuwa ya kipekee,hivyo wasubiri kwa hamu kubwa" alisema

 

video inatarajiwa kurekodiwa chini ya studio ya Black and White huku Audio ya wimbo huo ukirekodiwa na Studio ya  GML.

 


No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa