Thursday, April 15, 2010

AFRICAN LYON KUINGIA KAMBINI NA MCHEZO WA MWISHO
Baadhi ya wachezaji wa A.Lyon akimenyena na beki wa Simba SC moja ya mechi uwanja wa Uhuru Dar

Klabu ya soka ya African Lyon iliyobakia katika ligi kuu ya soka ya Tanzania Vodacom Premier League VPL, kesho inatalajia kuanza mazoezi kujifua kujiandaa na mchezo wao wa mwisho na JKT Ruvu ambao unaotalajiwa kuchezwa Jumatano hijayo Mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Klabu hiyo zilidai kuwa, timu hiyo inatalajiakuingia kuanza mazoezi hayo kesho.

"Kesho mapema tunatalajia kuingia mazoezini kujiandaa na mazoezi yetu,mazoezi hayo tunatalajia kufanyia uwanja wa Tanganyika Peckers, hivyo kocha anajiandaa kuwaatayarisha wachezaji kwa ajili ya mechi hiyo"  kilisema chanzo hicho cha Habari.

No comments:

Post a Comment

here u,re comments/acha ujumbe wako hapa